WAKATI IBENGE AIKINUKIA SIMBA….MASTAA HAWA 9 KUPIGWA PANGA MSIMU UKIISHA…

 


KLABU ya Simba itaachana na nyota tisa mwishoni mwa msimu huu akiwemo kipa mmoja, mabeki wawili, viungo wawili, mawinga wawili na washambuliaji wawili.

Imeelezwa kuwa wachezaji watakaotemwa baadhi ni wachezaji wa zamani na baadhi ya waliosajiliwa hivi karibuni kwa ajili ya kupisha wengine kusajili kuboresha timu hiyo kwa msimu ujao wa mashindano.

Taarifa za uhakika zilizotufikia kuwa viongozi wa klabu tayari wanatafuta wachezaji wa ubora wa juu ambao watasajiliwa na tayari majina matatu ambayo yamethibitishwa yapo kwenye meza ya kwa ajili ya kujadiliwa.

Chanzo hicho kimesema kuhusu kocha mpya anayekuja kuchukuwa nafasi ya Abdelhak Benchikha, upo katika mchakato huku baadhi ya majina yanajadiliwa.

“Moja ya jina limejadiliwa hivi karibuni ni Florent Ibenge wa Al Hilal ya Sudan, licha ya kuwepo kwa majina mengine, suala la Kibu (Dennis) uongozi unafahamu ushawishi kutoka kwa klabu fulani ambao wanataka kumsajili.

Kwa sasa ofa rasmi ya klabu inawasilishwa kuna mkutano na nyota huyo pamoja na viongozi umepangwa wiki ijayo kuongelea mustakbali wake lakini ni kuangalia na wachezaji wengine ambao mikataba yao imefikia tamati na kuongezwa,” amesema chanzo hicho.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema wanachokifany sasa ni kubaki na wale bora wenye moyo wa kuitumikia klabu hiyo.

“Dirisha hili la usajili tunaemtaka atabaki Simba lengo ni kutengeneza timu tishio turudi kwenye ufalme wetu,” amesema na aliongeza kuwa;

Licha ya timu yetu kusemekana ni mbovu lakini blndio timu inayoongoza wachezaji wake kuhitajika na klabu zingine ndani na nje , ni dhahiri kuwa tuna kikosi chenye wachezaji bora.

Hatujapata matokeo mazuri mdimu huu lakini haiondoi ukweli kuwa wachezaji wetu ni bor sana ndio maana wanatajwa sana sokoni,” amesema Munej huyo.

Ameleza kwa sasa nguvu zao wanazielekeza katika michezo iliyosalia kuhakikisha wanafanikiwa kumaliza nafasi ya pili ili kupata nafasi ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.