GAMONDI AFANYA KOSA HILI…MASHUJAA KUKUMBANA NA HILI…ISHU NZIMA HII HAPA

 


Kikosi cha timu ya Young Africans SC chenye wachezaji 20 na viongozi 11 wa benchi la ufundi wakiongozwa na Kocha Mkuu,

Miguel Gamondi, kesho Jumamosi kitasafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Kigoma.

Young Africans inaelekea Kigoma kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mashujaa FC utakaochezwa keshokutwa Jumapili kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani humo.

Wachezaji watakaosafiri ni makipa wawili; Djigui Diarra na Aboutwalib Mshery. Mabeki ni Ibrahim Bacca, Bakari Mwamnyeto, Kibwana Shomari, Dickson Job, Nickson Kibabage na Kouassi Attouhoula Yao.

Viungo ni Farid Mussa, Max Nzengeli, Mudathir Yahya, Khalid Aucho, Denis Nkane, Stephane Aziz Ki, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Sheikhan Ibrahim na Pacome Zouzoua, huku washambuliaji wakiwa Clement Mzize, Joseph Guede na Kennedy Musonda.

Mchezo huo wa mzunguko wa pili, Young Africans itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kushinda magoli 2-1 katika mzunguko wa kwanza, mchezo ukipigwa Februari 8, 2024.

Mbali na kuingia uwanjani kutokana na rekodi nzuri ya mzunguko wa kwanza dhidi ya Mashujaa, lakini Young Africans kwa sasa ndiyo vinara wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kufikisha pointi 62 kutokana na kucheza mechi 24.

Kuanzia sasa timu ya Yanga inahitaji pointi 11 pekee ili kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.