Matatizo ya Simba yanaanzia hapa, Mo Dewji Afanye hivi

 

Matatizo ya Simba yanaanzia hapa, Mo Dewji afanye hivi

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Farhan Kihamu amemshauri mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji 'Mo Dewji' kuweka mtu wake ndani ya klabu hiyo ili timu iweze kufanya vizuri.


Farhan amesema ikiwa kuna maneno yanayoendelea kuwa Mo Dewji ameikacha timu hiyo na hatoi pesa za kutosha kwa ajili ya usajili, ndiyo maana timu inafanya vibaya kwa miaka mitatu sasa.


"Arsenal pale kuna wakati mwenye timu yake Stan Kroenke alipotezea kabisa suala la kuipa timu mzigo wa kutosha mpaka pale Mwanae alipoichukua timu mambo yakabadilika tena na Mfanyabiashara yule Silent Stan akaanza kutia hela sana.


"Pale PSG mwenye mali yake Bwana Tamim Hamad Al Thani alipoinunua tu ile timu akamchukua Kijana kutoka kwenye biashara zake Nasser El Kherraffi akasimamie timu, Roman Abramovich pale Chelsea nae alimvuta Marina kutoka kwenye Kampuni zake na kumpeleka Stamford Bridge.


"Mwenye Mamelodi Sundowns, Bilionea Patrice Motsepe alipotoka tu akamweka Mwanae pale asimamie timu na biashara zote, hata Mfadhili wa Yanga, GSM amemweka Kijana wake pale Jangwani, Matajiri kiasili hawana shida ikitokea kwenye setup yenu yupo Mtu wake, hela hajiulizi mara mbili!


"Hata mwenye Man City, Sheikh Mansour amemweka Khaldoon Mubarak pale kama Mwenyekiti wa timu wala sio bahati mbaya.


"Anyways nilitaka tu kusema hata anguko la Leicester City ni baada ya tajiri kufariki kisha timu ikaenda kwa watu baki, ikashuka daraja na Mwanae alipoamua kurejea na kusimamia project imepanda tena Ligi Kuu kwa kishindo, nilitaka tu kusema hivyo! Matatizo huja pale tu ambapo TAJIRI hana Mtu wake kati yenu," amesema Farhan Jr.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.