Timu ya Simba Yafungwa Kibabe na Tanzania Prisons

 

Timu ya Simba Yafungwa Kibabe na Tanzania Prisons

Siku chache baada ya kufanikiwa kufuzu Hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, #Simba imejikuta ikipoteza furaha hiyo kwa kukubali kichapo cha magoli 2-1 dhidi ya #TanzaniaPrisons katika mchezo wa #LigiKuuBara kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro


Prisons imepata ushindi wake kupitia magoli ya Samson Mbangula dakika ya 45 na 64 huku Fabrice Ngoma akiifungia Simba dakika ya 89


Matokeo hayo yanairudisha Simba nyuma katika mbio za ubingwa kwa kuwa imesaliwa na pointi 36 katika mechi 16 ikiwa ni mchezo wa pili kupoteza msimu huu katika Ligi Kuu baada ya awali kupoteza dhidi ya Yanga, wakati Prisons yenyewe imefikisha pointi 27 katika michezo 19

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.