Kigogo TFF Afichua Ukweli wa Mkataba wa Dube na Azam FC, Kuna Milioni 700, Siasa Tupu

Kigogo TFF Afichua Ukweli wa Mkataba wa Dube na Azam FC, Kuna Milioni 700, Siasa Tupu

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Sheria na Wananchama wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Eliud Mvela, amesema kuwa, hakuna anayeufahamu mkataba wa mshambuliaji wa Azam FC, Prince Dube na klabu yake hiyo.

Mvela amesema kuwa huenda hata hizo Tsh milioni 700 wanazotaka Azam walipwe na Dube au klabu inayomtaka ili kuvunja mkataba, hazijaandikwa kwenye kipengele chochote cha mkataba jambo ambalo amesema kuwa ni siasa za mpira tu.

“Hakuna aliyeuona Mkataba wa Azam na Dube na kama Dube angeona mkataba ni wa thamani kubwa kuvunjwa asingeingia katika vita hii. Na kule anakotaka kwenda wameona mashariti ya mkataba yapo ndani ya uwezo wao.

“Inawezekana kauli za Tsh milioni 700 Azam wanaongea siasa tu lakini si ajabu hizo milioni 700 hazimo katika mkataba. Timu za Bongo mwisho wataishia kukaa chini na kumalizana kama ilivyokuwa kwa Feisal,” amesema Mvella.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.