Simba: Hatuhofii kucheza usiku

Simba: Hatuhofii kucheza usiku

.


Ahmed amefunguka hayo leo Marchi 20, 2024 alipokuwa kwenye uzunduzi wa hamasa za kuelekea mchezo wao dhidi ya Al Ahly utakaopigwa Marchi 29, 2024 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.


“Kwa ukubwa tuliokuwa nao hivi sasa hatuna wasiwasi na muda wowote wa mechi ambao tutapangiwa, sisi tuko tayari kucheza katika muda wowote na kupata matokeo. Kwa maandalizi tunayofanya tunakwenda kufanya vizuri. Mkulima hachagui jembe.”


“Niwakumbushe tu Wanasimba hii sio mara ya kwanza kucheza mechi usiku, tulicheza dhidi ya USGN muda wa saa 4 usiku na tukamfunga. Kwa maandalizi tunayofanya InshaAllah tunakwenda kupata matokeo.”


“Hakuna Mwanasimba ambaye anashindwa kwenda uwanjani saa 3 usiku kuangalia Simba yake. Mwanasimba wa kweli, mwenye mapenzi na timu yake, abayetaka kuipeleka timu yake nusu fainali hawezi kushindwa kwenda uwanjani saa 3 usiku. Hakuna Mwanasimba wa hivyo.”- Ahmed Ally


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.