Mashabiki wa Simba wapata ajali Vigwaza, mmoja afariki

Mashabiki wa Simba wapata ajali Vigwaza, mmoja afariki


Shabiki mmoja wa Klabu ya Simba amefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa kwenye ajali ya Basi dogo aina ya Costa lililobeba mashabiki wa Klabu hiyo lililokuwa likitokea mkoani Mbeya kuja Dar es Salaam kwenye mchezo wa robo fainali kugongana na roli eneo la Vigwaza alfajiri ya leo.


Mashabiki hao walikuwa wakitokea Tunduma kuja Dar es Salaam ambapo siku ya leo klabu hiyo ya Simba ina mchezo wa robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri ambao utachezwa katika Uwanja wa Benjamini Mkapa Dar es Salaam.


Tayari Kamanda wa Polisi Pwani wamefika eneo la tukio, taarifa zaidi kuhusu rukio hilo zitawajia baadaye.


Comments:

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.