Julio: Yanga wakicheza soka lao watashinda kwa Mamelodi

Julio: Yanga wakicheza soka lao watashinda kwa Mamelodi


Kocha Julio amesema Wananchi wana uwezo wa kuwashangaza Mamelodi na kwamba endapo wataupiga mpira mwingi kama ule uliowapa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria, itawamaliza kirahisi Wasauzi hao.


“Yanga ina kikosi imara sana, inacheza soka la kuvutia mimi nasema Yanga ikicheza kama ilivyocheza na Belouizdad itapata ushindi mkubwa, inatakiwa kurudia kucheza kwa kiwango kile mbele ya Mamelodi,” alisema Julio na kuongeza;


“Yanga hii naweza kuifananisha na ile Simba ya kina Luis Miquissone na Clatous Chama kabla ya kuuzwa mara ya kwanza, muunganiko wa wachezaji wao ni silaha kubwa mbele ya Mamelodi, ila wanatakiwa kushinda kwa ushindi mzuri ili msingi wa kufuzu kwao uanzie kwa matokeo mazuri ya kucheza nyumbani.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.