Klabu ya Simba imepata pigo baada ya mlinda mlango Aishi Manula kuripotiwa kupata majeraha yatakayomuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu kama ambayo yalimuweka nje mwanzoni mwa Msimu huu.
Manula anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kati ya miezi 10 hadi miezi 12.
Kukosekana kwa nyanda huyo wa timu ya Taifa ya Tanzania ni pigo kwa Wekundu wa Msimbazi, Simba SC kuelekea michezo muhimu ya hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika inayoanza kurindima kesho.
Simba Sc itachuana na Mabingwa watetezi, Al Ahly kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali leo Machi 29, 2024 katika dimba la Benjamin Mkapa saa 3:00 usiku.