Ubora wa Kikosi cha Yanga haujaja kwa kubahatisha

Ubora wa Kikosi cha Yanga haujaja kwa kubahatisha

Ubora wa Kikosi cha Yanga haujaja kwa kubahatisha

Moja kati ya kitu kilichopunguza ubora wa kikosi cha simba kwa miaka ya hivi karibuni basi ni sajili zao za wachezaji wa ndani ya nchi na nje ya nchi.


ukiangalia kwa upande wa yanga pamoja nao mara nyingine huwa wanafeli kwenye sajili zao ila wamekuwa sana wakifanikiwa kwa kusajili wachezaji walioko kwenye ubora tofauti na simba ambao wamekuwa wakifanya sajili ambazo hata mashabiki hawazielewi (za kubahatisha) hasa wa ndani.


mfano kwa miaka ya hivi karibuni simba imewajili Nassoro Kapama, Jimmyson Mwanuke, Hussen Kazi, Abdallah Hamis, Habibu Kiyombo, Mohamed Musa, miraj Athumani, ukiwatazama hawa wachezaji hata kwenye vilabu vyetu vya kati wanaweza wasipate nafasi ya kucheza.


kwa kipindi cha miaka 5 iliyopita ni mchezaji mmoja tu mzawa aliyesajiliwa na simba ambaye angalau ameweza kuingia kwenye kikosi cha simba (Kibu Denis)na kupata muda wa kutosha wakucheza huku Israel Patrick na baadhi ya wengine wakiwa na wakati mgumu wakupata nafasi za kucheza.


Ukiangalia kwa upande wa yanga wapo Bakari mwamnyeto, Dickson job, Kibwana Shomari, Mudathir Yahaya, Salum Abubakar, Ibrahim Bacca, Clement Mzize, Metacha Mnata, Abutwalib misheri, Kibabage wengi wao hata kama hawapati nafasi kwa sasa ila wanaubora.


Kuna hawa vijana wawili under 20 ambao wanafanya vizuri kwenye ligi yetu kwa sasa, lameck lawi(Coastal) na Ladack chasambi (Mtibwa sugar)sitashangaa Yanga wakiwasajili huku simba wakibaki kusajili wachezaji wa kubahatisha kila mwaka.


Pamoja vijana wetu wengi wakitanzania wamekuwa wanaonekana wanafeli wanaposajiliwa kwenye vilabu vyetu vikubwa kwangu mimi naona ni tofauti kwani naamini vilabu vyetu vimekuwa vikifanya sajili nyingi za kubahatisha bila kuangalia ubora.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.