Mchezaji Moses Phiri Kama Utani ndo Anakuja Hivyo Ligi Kuu

 
Mchezaji Moses Phiri Kama Utani ndo Anakuja Hivyo Ligi Kuu

Mchezaji Moses Phiri Kama Utani ndo Anakuja Hivyo Ligi Kuu

Moses Phiri, nyota wa Simba mdogomdogo anazidi kurejea kwenye ubora wake kutokana na kasi yake kwenye kufunga na kutoa pasi za mabao kuanza kuimarika.

Ipo wazi kwamba zama za kocha Roberto Oliveira hakuwa chaguo la kwanza katika kikosi hicho na mechi nyingi alianza kusugua benchi licha ya uwezo alionao.

Ni mabao matatu katupia ndani ya ligi akiwa ni namba mbili kwa wachezaji wenye mabao mengi ndani ya kikosi cha Simba.

Ni Jean Baleke yeye ni namba moja akiwa katupia mabao 7 msimu wa 2023/24. Phiri bao lake la tatu alitupia dhidi ya Ihefu alipoanzia benchi akitumia pasi ya Luis Miquissone ambaye naye alifikisha pasi yake ya tatu kwenye ligi.

Ikumbukwe kwamba msimu wa 2022/23 Phiri alitoa jumla ya pasi tatu za mabao na kufunga mabao 10. Tayari kafungua akaunti ya pasi za mabao alipotoa kwenye mchezo dhidi ya Namungo Uwanja wa Uhuru.

Pasi yake ya kwanza alitoa kwenye mchezo huo alipoanzia benchi pia na aliingia kipindi cha pili kutimiza majukumu yake wakati Simba ikigawana pointi mojamoja na Namungo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.