Alex Ngereza: Baleke wa Simba Anataka Kuhamia Yanga

 

Alex Ngereza: Baleke wa Simba Anataka Kuhamia Yanga


Alex Ngereza: Baleke wa Simba Anataka Kuhamia Yanga

Wakati huu ambao Yanga wanaonekana kukosa mshambuliaji sahihi wa kumrithi Straika wao alietimkia Misri Fiston Mayele.

Mchambuzi wa michezo kutoka TV3, Alex Ngereza anatuarifu kuwa Klabu ya Yanga inafanya umafia kwa majirani zao Simba kumnyakua Jean Baleke ambae kasi yake ya upachikaji mabao inaonekana kuwa tiba sahihi kwa safu ya ushambuliaji ya Yanga.

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Alex Ngereza ameandika;

"Nimearifiwa kwamba Jean Balake amepokea ofa nzuri kutoka Yanga na tayari amefanya mazungumzo na management yake waangalie kama wanaweza kuzungumza na uongozi wa TP Mazembe ili aweze kujiunga na Yanga dirisha dogo na kwa mujibu wa taarifa ni kwamba baleke ni pendekezo la Miguel Angel Gamondi"

Je unadhani ni kweli Baleke anatua mitaa ya Jangwani? Tupe maoni yako

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.