Nyota Watatu Simba Kwenye Vita Nzito wao kwa wao
Wachezaji watatu wanawania tuzo ya mchezaji bora ndani ya kikosi cha Simba kwa Septemba, 2023 ikiwa ni vita yao nyingine kumpata mbabe wao.
Ndani ya Septemba timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira ilifungua pazia la ligi kwa kupata pointi tatu muhimu.
Ilikuwa ni kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Manungu, Morogoro na ubao ukasoma Mtibwa Sugar 2-4 Simba.
Nyota waliongia kwenye orodha ya kuwania tuzo hiyo ni Shomari Kapombe, Che Malone Fondoh na Clatous Chama.
Kwa sasa kikosi hicho kipo Dar baada ya kutoka Singida kukamilisha mchezo wao wa ligi dhidi ya Singida Fountain Gate. Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Liti ubao ulisoma Singida Fountain Gate 1-2 Simba.