Ten Hag Hali Mbaya Man United, Mastaa Wafunguka Mazito, Wamtaja De Gea

 
Ten Hag Hali Mbaya Man United, Mastaa Wafunguka Mazito, Wamtaja De Gea


De Gea alikuwa kipa wa Manchester United kwa miaka 12 akiwa moja kati ya makipa bora.

Msimu uliopita, De Gea alitwaa Tuzo ya Golden Glove ndani ya Premier akiwa na clean sheet 17, huku akifanikiwa kuwa mchezaji bora wa mwaka kwa miaka minne ndani ya Man United.

Ripoti zinaeleza kuwa, baada ya De Gea kikosini hapo huku nafasi yake ikichukuliwa na Andre Onana, baadhi ya wachezaji wa Man United hawakukubaliana na jambo hilo.

Onana baada ya kutua hapo kwa pauni 50m, bado mambo hayajamnyookea ambapo katika mechi sita za kwanza, ameruhusu mabao 14.

Kipa huyo alinukuliwa akisema: “Haya ndiyo maisha ya kipa. Ni ngumu. Tulianza vizuri, lakini makosa yamekuwa mengi.”

Mbali na ishu ya kipa, pia sakata la Jadon Sancho kutengwa kikosini hapo linaonekana kuwakera wengi.

Sancho yupo nje ya kikosi hicho tangu Man United ilipopoteza dhidi ya Arsenal, hii ni baada ya kuonekana kumkosoa kocha wake kupitia mitandao.

Inaelezwa kuwa, kwa sasa ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo vya Man United, mambo hayasomeki, huku wachezaji wakikasirika kuhusiana na uamuzi wa kocha na upendeleo kwa baadhi ya wachezaji.

Kabla ya mechi ya jana dhidi ya Burnley, Ten Hag alipoulizwa kama Sancho atacheza, alijibu: “Inategemea, ila wengine wanajiandaa na mchezo, yeye hayupo kwenye kikosi.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.