Simba Yatolea Ufafanuzi Ajali Aliyopata Che Malone

Simba Yatolea Ufafanuzi Ajali Aliyopata Che Malone


Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amethibitisha kuwa ni kweli beki wao Che Malone Fondo amepata ajali leo Septemba 25 alfajiri akiwa anatoka uwanja wa ndege kupokea ndugu zake waliokuwa wamekuja kumtembelea.


Ahmed amesema kuwa tayari mchezaji huyo ameshakamilisha taratibu za hospitali na polisi na sasa ameruhusiwa kwenda nyumbani kupumzika.


Hata hivyo amesema Beki wao hajaumia kabisa (yupo fiti) katika ajali Ile aliyeumia ni kaka yake ambaye alipata michubuko kidogo.


"Ni kweli Che Malone amepata ajali leo maeneo ya mikocheni na hadi sasa ameshamaliza taratibu zote za hospitali na polisi na amekwenda nyumbani kupumzika"


"Hakuwa ametoka kula bata kama wengine wanavyosema," Simba inatarajia kutoa taarifa rasmi ya ajari hiyo muda mcheche kuanzia sasa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.