Kiungo Mshambuliaji wa Simba SC, Clatous Chama Alamba Dili la Ubalozi
"Nina furaha kuwajulisha kwamba nimesaini mkataba na @roby_sportswear ukiwa ni muendelezo wa ushirikiano wetu ambao tuliuanza miezi kadhaa iliyopita. Viatu vimekuwa ni sehemu muhimu kwenye utambulisho wangu, lakini pia kwa kila binadamu. Kwahiyo ushirikiano huu ni zaidi ya mimi kutangaza viatu tu, bali nitakuwa nafanya kitu ninachokipenda nje ya mpira.
Robby, endelea kutupendezesha ndugu yangu, sikukuu inakuja."