Ibrahim Bacca; Huu ni Muda wa Kwenda Ulaya Sasa

 

Ibrahim Bacca; Huu ni Muda wa Kwenda Ulaya Sasa

 Ibrahim Bacca; Huu ni Muda wa Kwenda Ulaya Sasa

Kwa sasa hapa nchini Ibrahim Bacca ni miongoni mwa mabeki bora wa kati wa Ligi Kuu na hata ukiweka orodha ya mabeki watatu bora basi huwezi kuacha kuweka jina lake.


Tangu asajiliwe na Yanga akitokea KMKM ya Zanzibar kiwango chake kimeendelea kukua maradufu na kupata nafasi ya kuitwa timu ya Taifa. Januari mwakani atakwenda AFCON yake ya kwanza pale nchini Ivory Coast.


Kwa sasa ana miaka 25 huu ndio wakati wake wa kwenda Ulaya kutafuta malisho mazuri zaidi ya anachokipata pale Yanga. Ni wakati sasa wanaomsimamia wamtafutie timu hata daraja la pili Ufaransa au kule katika Ligi kuu za Ulaya Mashariki.


Ibrahim Bacaa amekuwa bora mbele ya Bakari Mwamnyeto na Dickson Job ndio maana hata Kocha Miguel Gamondi huwa anamtumia Bacca kucheza na hawa wawili ila sio kuanza nje.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad