Simba SC Wampiga bei Joash Onyango

 

Simba SC Wampiga bei Joash Onyango

Uongozi wa Simba SC umetangaza rasmi kumuweka sokoni Beki kutoka nchini Kenya Joash Onyango Achieng kwa kuzitaka timu zinazomuhitaji kupeleka ofa mezani.


Onyango ni kati ya mabeki waliokuwa tegemeo katika msimu uliopita akiipambania timu hiyo katika Ligi ya Mabingwa Afrika na kufanikiwa kuifikisha hatua ya Robo Fainali.


Beki huyo mwenye umbo kubwa inadaiwa aliandika barua mara mbili ya kuomba kuondoka katika timu hiyo.


Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema kuwa wanakaribisha ofa kwa klabu yoyote itakayomuhitaji Onyango katika msimu ujao.


Ahmed Ally amesema kuwa, mara kadhaa Onyango anazushiwa kuandika barua ya kuondoka kitu ambacho sio kweli, huku akizitaka klabu zinazomuhitaji kuwasilisha ofa zao kwa uongozi.


Ameongeza kuwa hakuna ofa yoyote waliyoipokea hadi sasa ya kumuhitaji Onyango hivyo basi kama timu hiyo haitajitokeza ataendelaa kuichezea Simba SC.


“Hatuwezi kumzuia mchezaji atakayehitajika na klabu nyingine, kikubwa tutaangalia ofa kwanza kabla ya maamuzi mengine kufanyika.


“Hivyo tumetoa ofa kwa timu ambazo zinamuhitaji Onyango kuwasilisha ofa zao mezani kwa ajili ya kuzijadili,” amesema Ahmed Ally.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.