Team Job yawapa Tabasamu Wenye Uhitaji ikiifunga Team Kibwana

Team Job yawapa Tabasamu Wenye Uhitaji ikiifunga Team Kibwana


Ni mechi ya mabeki wawili wa Yanga Dickson Job 'Team Job' na Kibwana Shomari 'Team Kibwana' ikiwaunganisha mastaa na wadau wa soka nchini kucheza pamoja iliyomalizika kwa mikwaju ya penali 2-4 baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 leo katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

Team Job, ilipata bao dakika ya 22 na limefungwa Abdul Sopu nakuiwezesha timu yake kwenda mapumziko ikiwa kifua mbele dhidi ya wapinzania wao Team Kibwana 1-0

Kipindi cha pili Sopu ameongeza bao la pili na Team Kibwana kurudisha yote na mechi kumalizika kwa 2-2

Baada ya dakika 90 timu zilienda matuta na Team Job kuichapa Team Kibwana 4-2

'Wape Tabasamu' ni jina la tamasha hilo ambalo limelenga kusaidia Jamii yenye uhitaji na kurejesha tabasamu kwao.

Mchezo huo una lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia sekta ya afya kwa kuchangisha fedha kupitia mchezo wa soka hilo likiwa ni tamasha la pili baada ya kuzinduliwa mwaka jana katika uwanja wa Sabasaba na mchezo huo timu Kibwana ilikubali kipigo cha bao 3-0 yaliyofungwa na Simon Msuva bao mbili na Teps Evance.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad