Szoboszlai azingonganisha Liverpool, The Magpies

 

Szoboszlai azingonganisha Liverpool, The Magpies

Majogoo wa Jiji ‘Liverpool’ wamefanya mazungumzo na wawakilishi wa nyota wa RB Leipzig, Dominik Szoboszlai, lakini kifungu chake chenye thamani ya Puani 60 milioni inafikia kikomo leo Ijumaa (Juni 30).


Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alikiwasha Bundesliga msimu uliopita na pia Newcastle ilimtolea macho.


Kwa mujibu wa gazeti la Athletic, Majogoo wa jiji wamepania kumsajili kwenye dirisha hili la usajili japo uhamisho wake utakuwa mgumu kwa mujibu wa ripoti.


Kwa sasa Liverpool inasikilizia hadi kifungu chake cha pesa (Pauni 60 milioni) kimalizike kwa mujibu wa mkali wa masuala ya usajili Fabrizo Romano.


Sadio Mane: Nitaendelea kucheza Bayern Munich

Kwa hivyo Liverpool inataka dili likamilike haraka iwezekanavyo kabla ya RB Leipzig haijaongeza dau na kutibua mipango ya Jurgen Klopp.


Liverpool bado inafukuzia saini ya Kephren Thuram na Romeo Lavia ambao wametajwa kwenye dirisha hili la usajili la kiangazi.


Thuram, ambaye kwa sasa anakipiga katika kikosi cha Ufaransa chini ya umri wa miaka 21 kwenye michuano ya Europa, anakubalika sana Anfield, ingawa bado haijafahamika kama Nice itakuwa tayari kumuuza.


Wakati huohuo kinda Fabio Carvalho anakaribia kutia Leipzig kwa mkopo lakini dili lake halihusiani na staa huyo Szoboszlai.


Nyota huyo wa kimataifa wa Hungary ameiwakilisha timu yake ya taifa mara 32 na kuifungia Leipzig mara 10 msimu uliopita katika mechi 48.


FC Bayern Munich wang’ang’ana na Harry Kane

Newcastle inayonolewa na Eddie Howe nayo imevutiwa na staa huyo lakini itapata upinzani mkali kwa sababu Liverpool imepania kunasa saini yake.


Kocha huyo tayari amefanikiwa kunasa saini ya Sandro Tonali kwa Pauni 55 milioni kutoka AC Milan.


Liverpool inataka kuimarisha safu yao ya kiungo na tayari wamekamilisha uhamisho wa Alexis Mac Allister kutoka Brighton kwa Pauni 35 milioni.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.