Ngoja Nikwambia Simba Mpunga Upo, Watangaza Kuweka Kambi Uturuki

 

Ngoja Nikwambia Simba Mpunga  Upo, Watangaza Kuweka Kambi Uturuki
 Ngoja Nikwambia Simba Mpunga  Upo, Watangaza Kuweka Kambi Uturuki

Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wamegangaza kuweka kambi nchini Uturuki kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya 2023-24.


Simba wametangaza suala hilo leo Julai 3, 2023 kupitia Simba App ambapo wameweka wazi kuwa kikosi kinatarajia kuweka kambi nchini humo kwa wiki tatu kabla ya kurejea nchini mwishoni mwa mwezi huu.


Wamesema wakiwa nchini humo, wanatarajia kucheza mechi tatu za kirafiki ambapo kikosi cha Simba kikiongozwa na kocha Mkuu Roberto Oliviera pamoja na wachezaji wapya waliosajiliwa na wale wa zamani, kwa pamoja watapata utulivu wa kupeana mbinu mpya kisha kurejea nchini.


Mapema hii leo, kundi la kwanza la wachezaji 12 wa Simba walifanya vipimo vya afya huku ikielezwa kundi la pili linatataji kufanya vipimo hapo kesho.


Wachezaji waliofanya vipimo leo ni pamoja na Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr', Mzamiru Yassin, Israel Mwenda na Shomari Kapombe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad