Niwakumbushe tu Kidogo, Kocha Luc Eymael Alifurumushwa Tanzania Kwa Kauli za Kibaguzi

  

Niwakumbushe tu Kidogo, Kocha Luc Eymael Alifurumushwa Tanzania Kwa Kauli za Kibaguzi
Luc Eymael

Baada ya kusambaa kwa taarifa kuwa klabu ya Yanga imefunga kusajili kutokana na deni wanalodaiwa na aliyekuwa Kocha wao Luc Eymael, Yanga imemlipa kocha huyo.

Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe alikiri kuchelewa kwa malipo ya awamu ya mwisho ambayo sasa wameshakamilisha, Luc amethibitisha kuwa amelipwa.

"Robo tatu ya pesa wanazotakiwa kunilipa wamenipa, nashukuru kwa hilo kwa sababu nataka tumalizane kwa amani."

"Naipenda Tanzania kwani nilikuwa na wakat mzuri hapo, ni vile tu kulitokea changamoto, inabidi maisha mengine yaendelee," alisema.

Yanga ilifikia makubaliano ya kumlipa Eymael kwa awamu, baada ya kuvunja mkataba wake kutokana na kauli za kibaguzi.

Kocha huyo alifukuzwa nchini mwaka 2021 huku akipigwa marufuku kufundisha soka nchini Tanzania.

Afrika Kusini pia ilimzuia Eymael kufanya kazi katika nchi hiyo kutokana na matamshi yake ya kibaguzi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.