Klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini imethibitisha kumsajili mshambuliaji Ranga Chivaviro kutoka klabu ya Marumo Gallants iliyoshuka daraja.
Chivaviro (30) raia wa Afrika Kusini amesaini mkataba wa miaka miwili wenye chaguo la kuongezeka kwa mwaka mmoja zaidi.
Kupitia taarifa yake kwa umma Kaizer Chiefs imeandika:- “Tunapenda kuthibitisha rasmi usajili wa Ranga Piniel Chivaviro kutoka Marumo Gallants. Ametia wino kwenye karatasi baada ya kukubaliana na mkataba wa miaka miwili na chaguo la mwaka mmoja. Atavaa jezi maarufu #7”
Mshambuliaji huyo alikuwa akitajwa kuhitajika na Yanga na sasa ni dhahiri kuwa Yanga wamekosa huduma yake msimu huu.