Haji Manara Atoa BOKO 'Yanga inaweza Kuinunua Simba'

 

Haji Manara Atoa BOKO 'Yanga inaweza Kuinunua Simba'
Haji Manara

Kauli yenye kuudhi haswa, Yanga kuinunua Simba kutokana na utamaduni wa mpira wetu wa Tanzania ambao umegawanyika kwenye makundi makuu mawili, Simba na Yanga na tayari Haji Manara ameshaitoa kauli hiyo.


Manara ameandika mazito kwenye ukurasa wake wa Instagram akichagiza ripoti ya mapato na matumizi ya klabu ya Yanga ilisomwa juzi kwenye mkutano mkuu, kisha akagusa juu ya bajeti ya Yanga kwa msimu ujao ambayo inafika bilioni 20.


Manara alisema kama bajeti ya Yanga ni bilioni 20 kwa msimu ujao, thamani ambayo Mohamed Dewji (Mo) alisema atawekeza ndani ya Simba, hivyo Yanga wanaweza wakainunua Simba msimu ujao kwa kutumia bajeti yao ya msimu.


Manara aliweka video fupi kwenye Instagram yake ambayo inaonesha mtu mmoja akikinga mafuta sheli na kisha akanywa na kutoka nduki mithili ya pikipiki au gari na kisha akaweka ujumbe huo uliosema: “Hakuna shortcut katika kufanikiwa na lazma tubadilike.


“Tuishi kiuhalisia na tuache porojo, washabiki wetu wa leo sio wajinga wajinga na wamebahatika kuishi kwenye dunia ya teknolojia na mitandao ya kijamii. Tusiwe na akili ya huyo njemba ambae tunapigwa fix baada ya kunywa Petrol kama sio diesel katoka nduki kuliko Benz.”


Bajeti ya msimu ujao ya Yanga ni bilioni Ishirini, ni sawa na pesa ambazo Makolo (Simba) wameuza klabu yao hadi leo senti nyekundu hawajapewa yaani Kiufupi msimu ujao Yanga wanaweza kuacha kila kitu wakainunua FC kolo na kuigeuza klabu ya Pombe au kituo cha kujifunza ulevi.


Yote ni nini ? Ni uongo uongo tu na kutafuta shortcuts, kupenda kusifiwa upuuzi mitandaoni na kutafuta ukubwa wa fix wasiokuwa nao.


Hope jana (juzi) kuna fundisho kwa watu wa football, uongozi siyo lazma uongope na kuishi kwa ndoto za alinacha na itupe fundisho kubwa, kuendesha klabu ya mpira kunahitaji maarifa, sio umri mkubwa kama Unju bin Unuki.


Yanga bajeti yao ya msimu ulioisha ni kubwa zaidi ya bajeti ya timu ote za Ligi kuu ya Kenya na kama mjuavyo msimu ujao bajeti yao itakuwa kubwa maradufu.


“Kiufupi Dar es salaam Young Africans inaweza kuinunua Dunduka Fc na chenji ikabaki, Jumapili njema Wananchi, nyie wengine ajuae Mungu.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.