Adebayor Akutana na Viongozi wa Simba Kumalizana

Victorien Adebayor alikuwa na kikao na viongozi wa Simba SC kikao ambacho kilidumu kwa dakaika 40 ili kumshawishi Adebayor kujiunga na Simba SC,

Baada ya kikao kuisha taarifa zinaeleza kuwa Adebayor amekubali kuichezea Simba SC na atasaini mkataba wa miaka miwili kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.

Simba SC na Adebayor wamemalizana imebaki Simba SC waanze mazungumzo na RS Berkane ili kufikia makubaliano kumsajili Adebayor ambae amesisitiza kupewa nafasi ya kucheza kitu ambacho RS Berkane alikikosa

Winga huyo Vitorien Adebayor mwanye miaka 26 raia wa Niger 🇳🇪 huenda akawa sehemu ya kikosi cha Simba SC kitakachoweka Kambi mwezi ujao kujiandaa na msimu mpya 2023-24

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.