Haji Manara Afunguka Kuhusu Rais wa Yanga Kuvaa Jeans iliyochanika Chanika

Published from Blogger Prime Android AppHuyu ni Rais wa Club ya Mpira, huyu haongozi Chama Cha Siasa wala Kombania ya Wauza Magazeti, Na Good luck yupo safarini katika mazingira rafiki ya kuvaa Casual ya aina hyo

Umri pia unaruhusu kuvaa jeans za Vijana, Rais kijana hawezi kuvaa Misulupwete yenu wala Majampa, ukizingatia kazaliwa na kukulia town, huyu sio Mkalamba aliyekuja mjini na fuso la Viazi.na kuvaa ni Art kamili,, inayohitaji ujuzi na maarifa

Unategemea avae Suti katika mazingira ya leo wakati anajua Parade Inamhusu baadae? Lazma atupie Jeans kama kijana wa kileo anaeenda na fashion, Suti ina mahala pake na hawezi kila wakati kuvaa Suti na Tai ( auruke ujana Wake kisa Urais) Urais sio utumwa,,Urais haukuzuii kutupia mipigo yako,,na Urais sio full time misuti suti kama Afisa Tarafa

By the way ili uvae hvyo lazma uwe na Maji ya nguo, kama wewe Maji yako ya Mtoni hata uvae nini hupendezi

Nb:: Na huo Usela wake kasoma vzuri kuwazidi,,,Maarufu kuwazidi, Ana mzigo kuwazidi mabosi zenu, Mjanja kuwazidi, kisha anaongoza Club kubwa mara milioni ya Ofisi zenu Kwa kila kitu. Ni President wa Wananchi kijana mwerevu

@caamil_88
View all 879 comments
maimarthajesse 🔥🔥🔥🔥

1 DAY AGO
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.