Matajiri GSM Wafanya Kufuru Kubwa Yanga, Waweka Mzigo Mkubwa Kwa Wachezaji Yanga Ishinde Tena Afrika Kusini

GSM Wafanya Kufuru Yanga
Boss GSM/Yanga

Yanga jana ilikuwa uwanjani ikicheza mchezo wa kwanza wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini lakini matajiri wao kuna mzigo wa maana wa mtego wamewawekea mezani.

Matajiri wa Yanga kuna mabadiliko madogo wameyafanya katika mfumo wao wa bonasi za wachezaji ambapo sasa zitakuwa zikienda kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini tofauti na awali walipokuwa wanatoa ahadi ya mchezo mmoja kwenda mwingine.

Kwasasa Yanga inachofanya inatoa ahadi kwa mechi mbili za nusu fainali ile ya nyumbani na ugenini ambapo kama watafuzu kwenda fainali basi kuna kiasi cha sh 300 milioni mezani kwao.

Hii ina maana sawa na kusema kila mchezo mmoja utakuwa na thamani ya sh 150 milioni kwa timu hiyo ambapo wakivuka hatua hiyo watakuwa wamejihakikishia kiasi hicho cha fedha kutoka kwa matajiri wao wakiongozwa na mfadhili wao GSM.

Hatua tamu kwa timu hiyo ni kwamba ahadi za bonasi hizo zimekuwa zikitekelezwa kwa haraka vigogo hao wakitumia fedha hizo kupandisha mzuka kwa wachezaji wao katika mechi hizo kubwa.

Baada ya juzi jioni wachezaji kutangaziwa hivyo kuliibuka shangwe kubwa kwenye kikosi hicho huku wakisisitizana kuongeza umakini ili kushinda mechi hizo ambapo Yanga inavizia rekodi kubwa ya kucheza fainali ya shirikisho kwa mara ya kwanza katika uhai wa klabu hiyo.

Yanga msimu huu kwenye shirikisho imepoteza mchezo mmoja pekee dhidi ya US Monastir wakitoa pia sare mbili dhidi ya Real Bamako zote zikiwa mechi za ugenini wakati sare nyingine ikiwa ya nyumbani katika hatua ya robo fainali walipokutana na Rivers United. huku wakishinda jumla ya mechi tano mpaka hatua ya robo fainali.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.