Kocha mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuipongeza timu hiyo kushinda mechi ya kwanza nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Marumo Gallants ikishinda mabao 2-0.
Nabi raia wa Tunisia ametumia akaunti ya Instagram akiandika kwa kiswahili; "Asante sana Mama Samia",
Yanga jana pia baada ya ushindi ilipata Sh20 milioni za Rais Samia ambazo anatoa motisha kwa timu hiyo kwa kila bao likifungwa ananunua kwa Sh10 milioni.
Tazama hapa chini majibu ya Nabi kwa pongezi zilizotolewa na Rais Samia;