Marumo Wapatwa na Uoga 'Wafuta Viingilio Mechi dhidi ya Yanga"

 

Marumo Wapatwa na Uoga 'Wafuta Viingilio Mechi dhidi ya Yanga"

Marumo Gallants ya Afrika Kusini imetangaza hakutakuwa na kiingilio katika mechi ya marudiano nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Yanga Jumatano ijayo Mei 17 katika Uwanja wa Royal Bafokeng.


Marumo ilifungwa mabao 2-0 na Yanga jana Mei 10 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar.


Mchezo wa Nusu Fainali ya Mkondo wa pili baina ya Timu hizo utapigwa Mei 17 nchini Afrika ya Kusini.


Ikumbukwe kuwa Marumo Gallants pia walifuta viingilio katika mchezo wao wa Robo Fainali dhidi ya Pyramid FC ya Misri ambapo waliibuka na ushindi wa bao 1-0.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.