Avunjiwa Mkataba Ulaya Kisa Kwenda Kucheza AFCON

 

Younes Benali
Younes Benali

Klabu ya Nantes ya Ufaransa wameamua kusitisha mkataba wa mchezaji wa kimataifa wa Algeria, Younes Benali mwenye umri wa miaka 16 kwa sababu alisisitiza kuwa atarudi nchini kwake kucheza michuano AFCON ya U17.


Kauli ya Benali ambaye anamudu kucheza nafasi ya kiungo: "Tangu nikiwa mdogo, nimeichezea FC Nantes. Na kama wengi wanavyojua, ninaipenda klabu hii, ni klabu ninayoipenda sana. Nimekuwa nikiiheshimu, tangu nikiwa mdogo nilifanya kila kitu pale mpaka nilipata nafasi ya kuiwakilisha nchi yangu Algeria."


"Kutumikia Taifa langu ni fahari kubwa kwangu kwasababu hii haitokei kwa kila mtu. Nilifanya kila kitu vizuri Pamoja na klabu, Nilitii kila nilichopaswa kufanya. Sikuwa na dharau hata kidogo lakini tulishindwa kukubaliaba sehemu ndogo tu"


"Nilifanya uchaguzi wa kuheshimu nchi yangu na lazima iheshimiwe. Baadaye, wapo viongozi ndani ya klabu ambao hawakukubaliana na uamuzi wangu wakaamua kuvunja mkataba. Kwa sasa jambo la muhimu zaidi kwangu ni kufika mbali zaidi katika Kombe hili la Afrika."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.