Timu ya Azam |
KIKOSI cha Azam FC kimewasili usiku wa jana Mei 5 mjini Mtwara tayari kwa mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Simba SC Jumapili Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Azam baada ya kuwasili Hotelini hapo, Kaimu Afisa Habari wa Klabu hiyo, Hasheem Ibwe amesema kuwa kazi waliyoifata Mkoani humo ni kuondoka na ushindi tu na si vinginevyo.