Aidha ripoti hizo zinaeleza kuwa klabu ya Simba Queens ndio imetuma malalamiko hayo kwa TFF na baadae Shirikisho likatoa agizo hilo ili kupisha uchunguzi.
Hata hivyo Mukandayisenge alikuwa sehemu ya kikosi cha Yanga msimu uliopita na alicheza michezo ya Ligi akisajiliwa kutoka Rayon Sports ya Rwanda.
Alifunga goli kwenye mchezo dhidi ya Simba Queens uliopita.Mukandayisenge ndiye alikuwa kinara wa magoli kwenye mashindano maalumu ya Samia cup yaliyofanyika Jijini Arusha, akifunga magoli matatu (3).
Source; Edgar Kibwana