Tokea kujiunga kwake rasmi nawananchi 'YANGA' Julai 14 mwaka huu imekuwa vigumu sana kumuona kocha 'ROMAN FOLZ' akiwa anatabasamu au akicheka, kitendo ambacho kimetengeza majina mengi ya utani kwake na aina ya uchezaji wa timu yake.
Wapo walioita aina ya uchezaji wake 'PIRA MNUNO' nakuanza kukadiria siku zake zakuishi ndani ya kikosi hiko cha wanajangwani, wakiamini kuwa mashabiki waliowengi hawavutiwi na namna ya upatikanaji wa matokeo.
Baada ya tetesi na habari za kusadikika kuanza kusambaa juu ya ujio wa kocha alieifikisha timu ya Taifa ya 'MADAGASCAR' fainali za 'CHAN' kocha 'RAKOTONDRABE' almaarufu kama 'RORO' kuja kujiunga na kikosi hiko, wengi wakaamini kuwa ndio utakuwa mwisho wa kocha 'ROMAN FOLZ'
Kwakua miongoni mwa mahitaji ya kocha huyu mpya 'RORO' nipamoja na kuambatana na wasaidizi wake, akiwemo 'ASSISTANCE COACH' 'GOAL KEEPING COACH' na 'FITNES COACH' ambapo uongozi wa 'YANGA' umekubali.
Lakini ambacho kimekuwa kikiwachanganya watu ninamna Uongozi huo unavyomlinda kocha wao huku ukweli ukiwa wanakwenda kuleta kocha mpya ndani ya kikosi hiko.
Kumbe Kocha 'FOLZ' anakwenda kusimamia majukumu mengine, majukumu ya 'MKURUGENZI WA UFUNDI' huku walimu wa benchi lake la Ufundi, ikiwemo mwalimu wa magolikipa na mwalimu wa mazoezi (fitnes) wanaenda kuongeza nguvu katika benchi jipya la kocha 'RORO'
PUNGUZENI HUSDA, PIRA NUNO BADO LIPOLIPO SANAAA JANGWANI.