Kocha wa Yanga Apewa Thanks Klabu ya Ismaily SC




Ismaily SC yamfuta kazi kocha Miloud Hamdi baada ya matokeo duni

Klabu ya Ismaily SC kutoka nchini Misri imechukua uamuzi mzito wa kumtimua kocha wake, Miloud Hamdi, kufuatia mwenendo mbaya wa timu hiyo tangu aanze kuitumikia. Uongozi wa klabu hiyo umesema umefikia hatua hiyo baada ya kutoridhishwa na matokeo yasiyoridhisha yaliyokuwa yakizidi kuiweka timu katika hali tete kwenye ligi kuu ya Misri.

Tangu Hamdi alipokabidhiwa mikoba ya Ismaily, timu hiyo imecheza jumla ya michezo 11, lakini imefanikiwa kushinda michezo miwili pekee, sare moja, huku ikipoteza mechi nane. Matokeo hayo yameifanya Ismaily kushuka kwenye nafasi za chini kwenye msimamo wa ligi, jambo lililozua presha kubwa kutoka kwa mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kongwe.

Kwa sasa, uongozi wa Ismaily SC upo kwenye mchakato wa kumtafuta kocha mpya atakayeirudisha timu kwenye njia ya ushindi na kurejesha matumaini ya mashabiki. Wakati huo huo, kocha msaidizi amepewa jukumu la muda kuiongoza timu hiyo hadi pale atakapopatikana mrithi rasmi wa Miloud Hamdi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad