Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Madagascar Romuald Rakotondrabe Maarufu kwa Jina la Roro Huenda akatangazwa kuwa Kocha Mkuu wa yanga.
Jarida la L'Express De Madagascar Ndio limefichua Taarifa za Roro Kufanya mazungumzo Rasmi na young Africans na Mkataba aliopewa.
"Ni Klabu Bora zaidi Tanzania na moja ya zenye Mafanikio Afrika. Mambo muhimu katika Mkataba ni Pamoja na mshahara ambao Kabisa unaniridhisha. Kisha, Viongozi wa Klabu wameahidi kuhakikisha mahitaji yote ya Timu yanatimizwa kwa Hali Bora"
"Nitapewa Sehemu ya kukaa na Gari kwa ajili ya matumizi yangu ya KILA siku. Aidha nitaweza kusafiri mara mbili Kwenda Madagascar katika msimu mmoja kwa Gharama za Klabu "
"Hii ni Klabu ya Kitaalamu, KILA kitu kimepangwa Vizuri na kwa umakini " Jarida Hilo lilimnukuu Roro.
Tayari Young Africans Jana wametangaza kumfuta Kazi kocha Romain Folz Ambaye amedumu na yanga kwa Takribani Miezi Mitatu Tu.