HISTORIA imeandikwa, Azam FC imefuzu hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) kwa mara ya kwanza tangu klabu hiyo kuanzishwa miaka 21 iliyopita kufuatia ushindi wa jumla wa 9-0 dhidi ya KMKM Fc kwenye hatua ya pili ya CAFCC.
Azam Fc ilishinda 2-0 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza kabla ya kushinda 7-0 kwenye marudiano katika dimba la Azam Complex, Chamazi na kuandika historia hiyo.
FT Azam FC 🇹🇿 7-0 🇹🇿 KMKM FC (Agg. 9-0)
⚽️ 23' Idd Nado
⚽️ 27' Kitambala
⚽️ 30' Kitambala
⚽️ 43' Idd Nado
⚽️ 49' Msindo
⚽️ 53' Abdul Sopu
⚽️ 57' Abdul Sopu
.png)
