Mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC ambaye pia aliwahi kuzichezea Simba SC na Mazembe, Jean Baleke anatarajiwa kujiunga na Rayon Sports ya Rwanda kwa msimu wa 2025/2026.
Baleke aliondoka Yanga baada ya kushindwa kuwavutia benchi la ufundi la klabu hiyo msimu uliopita.
Ikiwa kila kitu kitakuwa sawa, Jean Baleke atasaini mkataba wa mwaka mmoja na Rayon Sports.