Mohammed Hussein Zimbwe Junior (Tshabalala) amehitimisha utumishi wake uliotukuka ndani ya Simba SC, Zimbwe ni legend pale Simba SC na amedumu kwa miaka 11.
Zimbwe anaondoka anaenda kujiunga na Yanga SC kwa ofa nono baada ya Simba SC kusuasua kuleta ofa inayoeleweka, kijana akafanya maamuzi sahihi kwa ofa sahihi, kwa nini nasema maamuzi sahihi sababu mpira ni kazi ya muda mchache sana ila bidi ukusanye mafao usije kuaibika.
Kama inavyosemekana ni ofa ya Mshahara wa Tsh milioni 25 kwa mwezi na ada ya usajili ya Tsh milioni 300 kwa Mkataba wa miaka miwili sio pesa mbaya maana yake Mkataba wake una thamani ya Tsh Milioni 900.
Simba SC wasipokuwa makini mwakani wataimba wimbo ule ule wa kujenga timu, Yanga kashinda karata muhimu sana wakati huu unaodaiwa MO Dewji amesusa ikidaiwa kuwa anataka pesa zake anazotoa Simba SC za ziada zitambulike kwanza kama Mkopo kwa Klabu ndio aendelee kutoa pesa, sawa na Yanga kumwaga petrol kwenye fukuto la nyasi kavu msituni muda wowote zinawaka.
Kama ni kweli basi usajili wa Zimbwe Yanga unakuwa umewalipa tayari kabla hata ya Zimbwe Jr kuanza kuwatumikia, kwa sababu ameondoka bure akiwa na kiwango bora, usajili ambao unaleta gumzo na kuchochea mgogoro/presha kwa Klabu kwa nini ameondoka? Yanga wanatuonea, tumekuwa wanyonge, kuna watu wanakula hela za MO, Mangungu anatuhujumu hadi paje kutulia Ligi imeanza na umefanya usajili wa presha ukizingatia Simba SC wameondoka wachezaji 9 hadi sasa (Zimbwe, Mavambo, Kijili, Okajepha, Kazi, Nouma, Ngoma, Omary na Manula, hapo hujui kama wamemaliza au laa.
Usajili wa Zimbwe ushawalipa Yanga SC kabla hata Zimbwe kucheza umewafanya mashabiki kujihisi unyonge kuondokewa na mchezaji mzawa wa kariba ya Zimbwe Simba SC ni pigo kwa