CLUB WORLD CUP FINAL
CHELSEA FC 🏴 3-0 PARIS SG 🇫🇷
⚽️ 22” Palmer
⚽️ 30” Palmer
⚽️ 43” Pedro
Rasmi sasa Chelsea ndio Mabingwa wa Klabu bingwa ya Dunia ,Yote kwa yote Robert Sánchez anakula mshahara wake kihalali kabisa
MIGOS ON STAGE " walk it , Talk it " wakati ambao dunia haikuamini wao waliamini. Wanaume wakaingia uwanjani na mentality ya kibingwa na bendera ya United kingdom mabeni.
Dunia ya mpira imechukua darasa jinsi ya kuwafunga na kuwanyanyasa PSG. Tatu bila kama TMK Family , kigeto-geto kama Juma Nature. Wakiuliza wale kina nina ? waambieni " Rastafarian Gang"
Watoto wa Paris kabla ya mchezo waliimba sana taarabu , wakasahau kuwa Metlife Stadium ni jukwaa la Hip Hop.
Mnaojiuliza alikuwepo wapi Vintinha ? Kamtafuteni kwenye mifuko ya Moi Caicedo, mtaalamu alikichukua kiungo chote, akatoa darasa la mpira na Vitinha amelielewa. Kwenu ilikuwa fainali, kwetu ulikuwa wa mapambano.
Yule Cole Palmer ni Lionel Messi wa London, mpira mwingi mguuni. Nyama zake laini kama ini , ila ni hatari kama papa baharini. Mabao mawili ya kiufundi sana, asisti ya viwango vya kidunia. What a player ?
Kila timu ni ngumu sana kama bado haijakutana na Chelsea, niwakumbushe tu ! Tuliwahi kuwachakaza Bayern Munich, Barcelona na Manchester City ya Pep Guardiola na sasa PSG wamelamba asali Yetu.
Historia imeandikwa na haiwezi kufutwa kamwe Kwa mara ya kwanza mashindano ya FIFA CLUB WORLD CUP kufanyika katika system mpya Chelsea imekuwa klabu ya kwanza kuchukua.