Rais Samia Kuwamwagia Taifa Stars Bilioni Moja Endapo Watachukua Kombe la CHAN

Rais Samia Kuwamwagia Taifa Stars Bilioni Moja Endapo Watachukua Kombe la CHAN


Samia Suluhu Hassan ametoa ahadi ya donge nono ya fedha taslimu Shilingi Bilioni 1 iwapo timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars watafanikiwa kutwaa Ubingwa wa CHAN 2024 ambayo yanafanyika mwaka huu kwa pamoja katika mataifa matatu ya

Tanzania, Kenya na Uganda.

Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Palamagamba Kabudi amesema Rais Samia ametoa ahadi ya kitita cha fesha Shilingi Billioni 1 endapo timu hiyo itatwaa ubingwa huo wa CHAN 2024.

“Katika kuchagiza hamasa kwa timu yetu ya Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa ahadi ya donge nono Shilingi Bilioni 1 kwa vijana wetu wa Taifa Stars wakifanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano haya ya CHAN 2024” amesema Waziri Kabudi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad