Kiungo nyota Mudathir Yahya bado hajasaini mkataba mpya na Yanga, licha ya klabu hiyo kumpa ofa ya Tsh. 100 milioni kama dau la usajili na mshahara wa Tsh. 10 milioni kwa mwezi akiona ni kama kushushwa thamani kabisa.
Hata hivyo, taarifa za ndani zinaeleza kuwa Mudathir amesita kusaini kutokana na ofa nono kutoka kwa watani wa jadi Simba SC ambao wameweka mezani Tsh. 150 milioni pamoja na mshahara wa Tsh. 15 milioni kwa mwezi.
Kwa sasa, nyota huyo yupo njia panda akichagua kati ya Jangwani na Msimbazi. Je, atavaa njano-kijani au nyekundu-nyeupe msimu ujao?