Mobile

MCHEZAJI Jonathan Ikangalombo Agoma Kutolewa Kwa Mkopo...

MCHEZAJI Jonathan Ikangalombo Agoma Kutolewa Kwa Mkopo...

Kiungo Mshambuliaji, Jonathan Ikangalombo ‘Ikanga Speed’ aliyeingia Yanga dirisha dogo, inadaiwa amewagomea mabosi wa klabu hiyo waliotaka kumtoa kwa mkopo Singida Black Stars akitaka wamvunjie mkataba jumla na kumpa chake vinginevyo aendelee kusalia kikosini hapo.

.

Awali arena tulidokeza taarifa Yanga ilikuwa mbioni kumtoa kwa mkopo Ikanga Speed kutokana na kushindwa kufanya maajabu tangu alipotua akitokea AS Vita ya DR Congo, lakini inaelezwa nyota huyo wa zamani wa DC Motema Pembe pia ya DR Congo amewachomolea dili hilo.

.

Inadaiwa, wasimamizi wa winga huyo, wameigomea Yanga kutaka kumtoa Ikanga Speed kwa mkopo badala yake wanataka uvunjiwe mkataba ili alipwe chake asepe jumla. Chanzo hicho kilisema uongozi wa mchezaji huyo hautaki apelekwe kwa mkopo ila mkataba wa miaka miwili uliosalia uvunjwe, ili kila mmoja aendelee na yake.

.

Kiungo mshambuliaji huyo anayemudu wingi zote mbili alijiunga na Yanga Janutai 16 mwakahuu kwa mkataba wa miaka miwili na nusu na tayari ameshatumikia nusu mwaka na imesalia miwili.

.

“Makubaliano yaliyofanyika hadi sasa ni Ikangalombo ataendelea kusalia Yanga, maana uongozi haupo tayari kuvunja mkataba wa miaka miwili kwani ingelazimika kulipa pesa ndefu, lakini usajili unaendelea lolote linaweza likatokea,” kilisema chanzo kutoka ndani ya Yanga na kuongeza

.

“Yanga tunaleta kocha mpya atakayekuja na machaguo yake na mifumo yake, hivyo kunaweza kukawa na mabadiliko ya kikosi akianza majukumu yake kila kitu kitakaa katika mstari, tutajua nani wanaondoka na nani wanaingia ila kwa sasa ni Ikangalombo bado yupo sana Jangwani.”

.

Tangu atuje Yanga, Ikangalombo amecheza mechi sita za Ligi Kuu akitumia dakika 136 akiasisti mara mbili, bila kufunga bao lolote, japo katika Kombe la Shirikisho (FA) alifunga moja katika hatua ya 16 Bora walipoifunga Songea United kwa mabao 2-0.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad