Khalid Aucho Aongezewa Mkataba Yanga, Bado Yupo Sana

Khalid Aucho Aongezewa Mkataba Yanga, Bado Yupo Sana


Mabingwa wa nchi, Young African imemaliza utata kwa kiungo mkabaji, Khalid Aucho 🇺🇬 kwa kumpa mkataba wa mwaka mmoja ili aendelee kusalia klabuni hapo.


“Tunaheshimu mchango wa Aucho ambaye uzoefu wake unaonekana uwanjani, hivyo uwepo wake, kuna kitu kikubwa kitaendelea kuongezeka katika eneo la kiungo,” kilisema chanzo hicho.


Aucho alikuwa ni miongoni mwa wachezaji waliomaliza mikataba na klabu hiyo na mabosi wameanza naye kwa kumpa mkataba huo mpya wakiendelea kuzungumza na wengine ili kuwabakisha wakati, ikielezwa kocha mpya atakayechukua nafasi ya Miloud Hamdi tayari yupo nchini akiwa amesaini mkataba na bado kutambulishwa tu.


Ingawa Yanga wamefanya siri, lakini kocha huyo mpya ni Mfaransa Julien Chavelier aliyekuwa akifundisha Asec Mimosas

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad