Aliyekuwa kocha wa Wydad Casablanca, Rolani Mokwena ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa Mabingwa wa Ligi Kuu ya Nchini Algeria (Ligue 1), MC Alger baada ya kutupiwa virago na Wydad mnamo Mei 20, 2025 akichukua mikoba ya Mtunisia, Khaled Ben Yahiam
Mokwena (38) raia wa Afrika Kusini ambaye amewahi kuinoa Mamelodi Sundowns kwa mafanikio makubwa amesaini mkataba wa miaka miwili na anatarajiwa kuiongoza MC Alger kwenye msimu ujao wa mashindano ikiwemo michuano ya klabu Bingwa Afrika.