Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga Sc, Kennedy Musonda ametambulishwa kama mchezaji mpya wa klabu ya Hapoel Ramat Gan ya Nchini Israel kwa mkataba wa mwaka mmoja na chaguo la ongezeko la mwaka mmoja zaidi akitokea Young Africans Sc.
Hapoel Ramat Gan ambao ni Mabingwa wa Ligi Kuu Nchini Israel msimu wa 1963-64 kwa sasa wanashiriki Ligi Daraja la Pili Nchini humo almaarufu ‘Liga Leuit’