Kocha Miloud Hamdi Aondoka Yanga Licha ya Mafanikio ya Makombe
Aliyekuwa Kocha wa Yanga SC, Miloud Hamdi amejiunga na Ismaily SC ya Egypt 🇪🇬 kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Kocha Miloud Hamdi anajiunga na Ismaily na makocha wawili wasaidizi Hammadi Saghier Kocha Msaidizi raia wa Belgium na Marouane Silimani Kocha wa viungo (Fitness Coach) kutoka nchini Tunisia.
Kocha Miloud Hamdi msimu huu akiwa kama kocha wa Yanga SC amebeba makombe matatu, Kombe la Muungano, Kombe la Ligi Kuu ya NBC na Kombe la CRDB Bank.
Ismaily SC inamlipa Miloud Hamdi mshahara mara mbili zaidi na aliokuwa anapata Yanga SC, Ismaily SC watamtangaza leo Kocha Miloud Hamdi