Klabu ya Chelsea imetinga hatua ya fainali ya michuano ya Kombe la Dunia la klabu inayoendelea nchini Marekani.
Chelsea imetinga hatua hiyo baada ya kuitandika Fluminense mabao 2-0.
Hata hivyo, nusu fainali ya pili itacheza leo kati ya PSG na Real Madrid mchezo utakaochezwa saa 4:00 Usiku, kumtafuta mshindi atakayecheza dhidi ya Chelsea