Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu ya Tanzania bara, Klabu ya Young Africans Sc (Yanga) leo Jumatano Julai 23, 2025 imemtangaza Romain Folz kama Kocha Mkuu wake.
Kupitia Ukurasa wa Klabu hiyo wa Instagram, Young Africans imechapisha picha za Folz na kuandika "The Boss has arrived" huku chapisho lingine la Video likimuonesha Folz akijitambulisha kama Kocha Mkuu wa Kikosi hicho kinachojiandaa na msimu ujao wa ligi pamoja na usajili wa wachezaji wapya