Cole Palmer MVP wa Kombe la Dunia 2025

Cole Palmer MVP wa Kombe la Dunia 2025



Kiungo mshambuliaji wa Chelsea, Cole Palmer ameshinda tuzo ya mchezaji bora (MVP) wa michuano ya kombe la Dunia la FIFA ngazi ya klabu baada ya kuisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa kombe hilo.

Palmer amekabidhiwa tuzo hiyo na Rais wa Marekani, Donald Trump baada ya kuchangia jumla ya magoli 5 kwenye mechi saba za michuano hiyo akifunga magoli matatu na kusaidia ‘assist’ mengine mawili.

Nyota huyo raia wa England amehusika kwenye magoli yote matatu kwenye ushindi wa 3-0 dhidi ya Paris Saint-German kwenye fainali akifunga magoli mawili na ‘assist’ moja.

Mshambuliaji wa Real Madrid, Gonzalo García ameshinda tuzo ya mfungaji bora wa michuano hiyo baada ya kufunga magoli manne wakati winga wa PSG, Désiré Doue alichaguliwa kuwa mchezaji bora chipukizi huku golikipa wa Chelsea akishinda tuzo ya kipa bkta wa mashindano.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad