BREAKING: Dewji MO Kutoa Tamko Muhimu Leo Usiku

BREAKING: Dewji MO Kutoa Tamko Muhimu Leo Usiku

Mwekezaji na Rais wa heshima wa Simba SC, Mohammed Dewji (MO) ametangaza kuwa leo July 14 2025 saa nne usiku atatoa tamko muhimu.

Katika chapisho lake fupi katika mitandao ya kijamii, Mo hajadokeza ni kitu gani atachokwenda kukizungumzia hiyo saa nne lakini bila shaka itakuwa ni kuhusu Simba ambapo chapisho lake limesomeka “Wana Simba leo saa 4:00 usiku (EAT) nitatoa tamko muhimu, tukutane hapa”

Itakumbukwa June 02,2025, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally aliwaomba Wapenzi wa Simba kuwa na subira kutokana na kukosa ubingwa akisema ukubwa wa Afrika ndio kitu wanachokitafuta kwa sasa na hawapo mbali kufikia huku akiwasisitiza waiunge mkono Simba bila kuchoka na wamuunge mkono Mwekezaji Mo Dewji kama walivyofanya PSG na Pyramids kwa Wawekezaji wao ambao walilazimika kusubiri miaka 6 na mwingine miaka 14 ya uwekezaji ndipo wakatwaa ubingwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad